Joshua 3:1-5 Joshua
anawaambia wana wa Israeli kuchukuwa hatua ili kuweza kukabili safari
iliyokuwa mbele yao kwa kuwa wanatakiwa wajitakase ili waweze kuanza
safari.ili uweze kufanikiwa
ni lazima uchukue hatua ya kutenda au kukabili jambo husika ambalo
unatalaji
kulifanya,hivyo tunatakiwa tuchukue hatua katika neno ili tuweze
kushinda vita
vinavyo tukabili ,na Mungu anatusubili sisi aone kama tunatii neno lake
kwa
kuchukua hatua ili aweze kushusha Baraka zake juu yetu.
Kutoka 2:11-15 Jitahidi
kuangalia hali uliyokuwa nayo kisha
angalia yale unayoyafanya kama kweli
yanaendana na neno la Mungu linavyotuonya na kutufundisha,na kama sivyo basi chukua hatua ya kujirekebisha ili Mungu
akutendee,wakristo wengi wanajifariji
kwa kuomba maombi marefu, kuhudhulia
kwenye ibada kila siku,lakini wanasahau kuwa Mungu anapendezwa na
wanaotii neno lake na kukubali kutubu,kwa kughaili na kuacha maovu na kutenda
mema.Kutoka 3:6 acha kujifariji kwa
kuigawa dhambi ukidhani kuna kubwa na ndogo,elewa kwa Mungu zote ni dhambi kwa kuwa zinampeleka
mtu jehamu.Kutoka 5:1 licha kuwa utachukuwa hatua sio
kwamba mambo yatakuwa mazuri
hapana, inawezekana yakawa magumu sana ,kama ilivyokuwa kwa Musa na
Haruni wakati Mungu anasema nao juu ya kwenda kwa Farao kuomba kibali cha wana
wa Israeli kwenda kumwabudu Mungu wao.kutoka 5:1-12 tunapochukuwa hatua bwana
anajidhibitisha kwetu,zipo hatua zinazotufaa sisi tuzichukue ili kuweza kupona.
· Chukua
hatua ya kuliamini neno la Mungu.Kutoka
14:13-16,wakristo walio wengi
wanashidwa kwa kuwa wanakuwa mafundi wa kusikiliza na kuandika mafundisho yote
yanayofundishwa,lakini ndani yao kumejaa
mwalakini na kutoamini kuwa maneno
yanayosemwa au ahadi zilizotolewa na Mungu kuwa ni kweli ,tunakuwa
wagumu wa kuamini tunasubili mpaka tuone
ndipo tuamini ,yapo mengine hatutapokea endapo hatutaruhusu kuamini ndani yetu.
· Chukua hatua ya kutenda.yapo mafundisho ya Mungu
ambayo yanatufundisha kuamini neno la
Mungu ili tuweze kupokea Baraka ,lakini waliowengi ndani yetu tumekuwa na
mashaka juu ya kile ambacho tunakiomba na matokeo yake watu hawapokei kwa kuwa
ndani yao yamejaa mashaka mengi.Musa
anaambiwa na Mungu juu ya kuwaongoza wana Israeli afanye tendo la imani la
kupiga fimbo juu ya bahari na Musa alipochukua hatua bahari iligawanyika na
wakapita salama,je? endapo angekuwa na mashaka wangevuka? Matendo 12:1…,Hesabu 13:1-3
· Chukua hatua ya kuhakikisha kile unachoambiwa.katika nyakati hizi tulizo nazo ni ngumu na mbaya sana kama
hatutachukuwa hatua za kumkariba Mungu
ili atusaidie,kwa sasa wapo watu wanaojiita
kuwa ni manabii na mitume na mafundisho
wafundishayo siyo mazuri kwetu ,hivyo
inatakiwa kuhakikisha kile unachojifunza
kama kweli ni chema mbele za Mungu na utaweza kuhakikisha kwa kusoma neno na
kumruhusu roho mtakatifu atufunulie na kutufundisha.
· Chukua hatua ya kumng’ang’ania Mungu Kutoka 33:1-6 licha ya kuwa Musa alimg’ang’ania Mungu si kwa kutaka mahusiano
mema na Mungu bali alitaka pia ushilika na yeye,hivyo na wewe usikubali kuondolewa au kujiondoa mbele za Mungu
pasipo kupokea kile ambacho
umeahidiwa wewe ukipate,ng’ang’ania kwa Mungu ili ashilikiane nawe
katika hali zote na majira yote na yeye endapo
utayatoa maisha yako kwake, atakupa yale yanayokufaa.
Joshua23:6
inawezekana kabisa imani zetu ni kubwa sana
lakini kama katika matendo hatufanyi inavotupasa basi imani zetu ni
mfu,kwa kuwa neno la Mungu linasema imani pasipomatendo imekufa,Yakobo 2:14,17 unaposikia neno la Mungu
epuka mizaha na kulichukulia mazoea
na uchukue hatua ya kulitendea kazi ,kwa kuwa kuna mambo huwezi kupata
au hayawezi kuondoka yenyewe usipochukua hatua wewe mwenyewe,na ukichukua hatua
Mungu ni mwema kwetu atatutendea na atatupa Baraka.Ameen.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni