Ijumaa, 3 Julai 2015

Wokovu maana yake nini?


        Wokovu maana yake nini?


Inawezekana una maswali kama haya ndani ya moyo wako. Nini maana ya kuokoka? Au wokovu maana yake nini? Na ninawezaje kuokoka nikiwa hapa duniani? au ni kwanini niokolewe? Au nitaokolewaje? Swali lingine ambalo inawezekana unalo ni hili nikiisha kuokoka nifanye nini au nitaishije nikiwa hapa duniani?
Nimekutana na watu wengi sana wanaposikia habari hii ya kuokoka, wamekuwa na maswali kama haya mioyoni mwao, na nilipokupa wewe hii nafasi ya kukoka ninajua kuwa utakuwa na maswali kama haya moyoni mwako, ndio maana nimeamua kukujulisha kwa ufupi maana ya wokovu, na ni kwa nini unatakiwa uokoke na ukiisha kuokoka unapaswa uishije nimemwomba Roho Mtakatifu anisaidie kukiachilia kwa ufupi kile alichokiweka moyoni mwangu kinacho kuhusu habari za wokovu. Tafadhali Gonga Hapa kwa habari kamili juu ya wokovu. Baada ya kuokoka unahitaji msaada wa mafundisho juu ya wokovu.

Sala ya Toba

“Ee Mungu wangu ulie Mtakatifu. Ninakuja mbele zako. Mimi ni mwenye dhambi. Naomba unisamehe dhambi zangu zote nilizokukosea katika maisha yangu. Ninatubu kweli. Naomba damu ya Yesu Kristo iliyomwagika msalabani kwa ajili yangu initakase sasa katika roho yangu na nafsi yangu na mwili wangu. Nimefungua moyo wangu. Bwana Yesu Kristo nakukaribisha ndani yangu. Ingia kwa uwezo wa Roho wako – uwe Bwana na Mwokozi wangu kuanzia sasa na siku zote. Ahsante kwa kunisamehe na kwa kuniokoa. Nimejitoa kwako nikutumikie katika siku zote za maisha yangu. Shetani hana mamlaka tena juu yangu katika jina la Yesu Kristo. Amina.”

Nini cha kufanya?

questions_0000_Layer-3Inawezekana sasa una swali kama hili moyoni mwako, nifanye nini ili niokoke? Swali hili limewahi kuulizwa na watu wengi miongoni mwao ni huyu askari, alimuuliza Mtume Paulo afanye nini ili apate kuokoka, “Kisha akawaleta nje akasema, Bwana Wangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? Wakamwambia, mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako” (Matendo 16:30-31). Ili leo hii uokolewe unapaswa Umwamini Bwana Yesu, swali umwamini kama nani? Unatakiwi umwamini kama Bwana na mwokozi wako, sikiliza, unaweza kabisa ukawa na imani kwa Yesu kama Mfalme, kama nabii, nk, lakini ukawa hauna imani kuwa Yesu ndiye mwokozi wako, pia unaweza ukawa na imani kuwa Yesu ni mwokozi, lakini ni mwokozi wa watu wengine, wewe bado haujampokea kama mwokozi wako, fahamu unatakiwa umpokee wewe kama mwokozi wako kwa kumuamini kuwa alikuja kwa ajiri yako, tunaupokea wokovu huo kwa njia hiyo ya imani. Imani maana yake ni kuwa na hakika na jambo lile unalolitalajia ambalo halijaonekana kwa macho haya ya nyama “Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo ni bayana ya mambo yasiyoonekana” (EBR 11:1) na imani huja kwa kusikia neno la Kristo “Basi imani chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.” (WARUMI 10:17).
Neno la Kristo lina sema wazi kuwa ukimwamini Bwana Yesu utaokoka, Amini leo, kuwa Yesu Kristo ndiye mwokozi wa maisha yako, utakapo amini na kuamua kukipokea hicho ulicho amini fahamu, leo hii Yesu Kristo atavunja kiambaza kile kilichokuwa kimewatenganisha au kwa lugha nzuri kifo, kifo hicho ninachokizungumzia ni kile cha rohoni, amini atakuja kwako sikia anavyo sema “Tazama nasimama mlangoni nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango,nitaingia kwake,nami nitakula pamoja naye,na yeye pamoja nami.” (UFU 3:20)
Ukiamini au ukiwa na uakika wa maneno haya na unaamua kuufungua mlango yaani kukubari kumluhusu aingie ndani yako fahamu ataingia,na utakuwa na ushirika naye kabisaa, Je! Upo tayari Kuokoka leo hii? Kama upo tayari basi fanya hivi, tafuta pahali patulivu kisha ikiwezekana piga magoti, tafakari kisha sali sala ya toba ifuatayo kwa sauti

Hakuna maoni:

Unordered List

Download

Contact Us

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *