Katika mwongozo huu tunaona jinsi maombi yanavyotusaidia kujenga
uhusiano wenye nguvu zaidi pamoja na maisha ya Kikristo yenye nguvu.
1. Kuzungumza Na Mungu
Je, tunawezaje kuwa na uhakika kwamba Mungu anatusikia tunapoomba?
"Ndipo mtaniita mimi na kwenda KUNIOMBA, nami NITA SIKILIZA. Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote." - Yeremia 29:12,13.
"Ndipo mtaniita mimi na kwenda KUNIOMBA, nami NITA SIKILIZA. Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote." - Yeremia 29:12,13.
Je, ni uthibitisho gani aliotoa Yesu kuonyesha kwamba atasikia na
kujibu maombi yetu?
"Basi nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, na mlango utafunguliwa kwenu." - Luka 11:9.
"Basi nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, na mlango utafunguliwa kwenu." - Luka 11:9.
Maombi ni maongezi ya pande mbili. Hii ndiyo maana Yesu anaahidi
anasema:
"Tazama nasimama mlangoni, nabisha. Mtu ye yote akiisikia sauti yangu, na kuufungua malngo, nitaingia na kula pamoja naye, na yeye pamoja nami." - Ufunuo 3:20.
"Tazama nasimama mlangoni, nabisha. Mtu ye yote akiisikia sauti yangu, na kuufungua malngo, nitaingia na kula pamoja naye, na yeye pamoja nami." - Ufunuo 3:20.
Kwa jinsi gani inawezekana kwetu kuketi na kuwa na maongezi mazuri
wakati wa chakula cha jioni pamoja na Kristo? Kwanza, kwa kumwambia kila kitu
tulicho nacho moyoni mwetu kwa njia ya maombi. Pili, kwa kusikiliza kwa makini.
Tunapotafakari wakati wa maombi, Mungu anaweza kuongea nasi moja kwa moja. Na
tunapolisoma Neno la Mungu kwa roho ya ibada, Mungu ataweza kuongea nasi
kupitia katika kurasa zake.
Maombi yanaweza kuwa njia ya maisha kwa Mkristo.
"OMBENI BILA KUKOMA; shukuruni kwa kila jambo, maana hayo
ndiyo mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu." - 1 Wathesalonike
5:16-18.
Je! sisi tunawezaje "kuomba bila kukoma?" Je, yatupasa
kupiga magoti wakati wote au kurudia-rudia kusema maneno ya kumsifu au kutoa
dua? La, hasha. Lakini tunapaswa kuishi karibu sana na Yesu kiasi cha kujisikia
huru kusema naye wakati wo wote, na mahali po pote.
"Tukiwa katika makundi ya watu mitaani, katika shughuli ya
kibiashara, tunaweza kutoa dua yetu kwa Mungu na kumsihi atupe uongozi wake…
Daima tungeacha wazi mlango wa moyo wetu na kuuacha mwaliko wetu ukipanda juu
ili Yesu aweze kuja moyoni mwetu na kukaa humo kama mgeni wetu wa
mbinguni." - Steps to Christ, uk. 99.
Mojawapo ya njia bora sana ili kujenga uhusiano huo wa karibu sana
ni kujifunza kutafakari wakati tunapoomba.
"Kutafakari kwangu na kumpendeze yeye, mimi ninapomfurahia
BWANA." -Zaburi 104:34.
Unapoomba usiharakishe tu kupitia orodha ya mambo unayotaka.
Ngojea. Sikiliza. Kutafakari kidogo ukiwa katika maombi kunaweza kuuboresha
sana uhusiano wako na Mungu.
"Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi." - Yakobo
4:8.
Kadri sisi tunavyozidi kumkaribia sana Yesu ndivyo kadri
tunavyoweza kuonja kuwako kwake. Basi wewe unapaswa kuwa katika umbali wa
kuweza kuongea na Yesu, wala usiwe na wasi wasi juu ya kusema maneno yaliyo
sahihi. Ongea tu naye kwa unyofu wa moyo na bila kuficha kitu. Ongea juu ya
kila kitu. Yeye amepitia maumivu makali sana ya kifo kile chenyewe ili apate
kuwa Msiri wako.
2. Jinsi Ya Kuomba
Tunapoingia katika maombi, tunaweza kupenda kufuata muhtasari wa
sala ya Bwana, sala ya mfano ambayo Yesu aliwafundisha wanafunzi wake kuitikia
ombi lao hili:
Tufundishe sisi kuomba.
"Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe, ufalme wako uje, mapenzi yako yatimizwe hapa duniani kama huko mbinguni. Utupe leo riziki yetu. Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tulivyowasamehe wadeni wetu. Wala usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu, kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina" - (Mathayo 6:9-13).

Kulingana na mfano huo ambao Yesu aliutoa katika sala yake, sisi
tunatakiwa kumwendea Mungu kama Baba yetu aliye mbinguni. Tumwombe kwamba
mapenzi yake yatawale mioyo yetu kama vile mapenzi yake yanavyotawala katika
mbingu yote. Tunamtafuta ili atupatie mahitaji yetu ya kimwili, msamaha wake,
kwa ajili ya kuwa na roho ya kuwasamehe wengine.
Kumbukeni ya kwamba uwezo wetu wa kuipinga dhambi unatoka kwa
Mungu. Sala ya Kristo inahitimisha kwa maneno ya sifa kwake.
Safari nyingine Yesu aliwafundisha wanafunzi wake kumwomba Baba
"kwa jina langu" (Yohana 16:23) - yaani, kuomba kulingana na kanuni
zake Yesu. Hii ndiyo maana Wakristo kwa kawaida hufunga sala zao kwa maneno
haya: "Katika jina la Yesu, Amina." Amen (amina) ni neno la Kiebrania
limaanishalo "Na iwe hivyo".
Japokuwa sala ya Bwana inatoa mwongozo juu ya mambo tunayotakiwa
kuyaomba na jinsi ya kutunga sala, mawasiliano yetu na Mungu yanakuwa bora sana
kama yanatoka moyoni mwetu kwa hiari.
Tunaweza kuomba juu ya kila kitu. Mungu anataka tumwombe msamaha
kwa dhambi zetu (1Yohana 1:9), tumwombe atuongezee imani (Marko 9:24), tumwombe
uponyaji wa maumivu na magonjwa yetu (Yakobo 5:15), na kumwagiwa kwa Roho
(Zakaria 10:1). Yesu anatuthibitishia kwamba tunaweza kumpelekea yeye mahitaji
yetu yote, pamoja na mashaka yetu; mno kuweza kumwomba.
("Mwekeeni matatizo yenu yote, maana yeye
anawatunzeni") - 1 Petro 5:7.
Mwokozi wetu anapendezwa na mambo yo yote madogo yahusuyo maisha
yetu. Moyo wake huchangamka wakati inapomwendea mioyo yetu kwa upendo na imani.
3. Maombi Ya Faragha
Wengi wetu tunayo mambo fulani ambayo tunasita kuwaambia hata
marafiki zetu wa karibu sana. Kwa hiyo, Mungu anatualika sisi kuutua mzigo huo
katika maombi yetu ya faragha: tukiwa kila mmoja peke yake na yeye. Si kwamba
yeye anahitaji maelezo yote. Mwenyezi anajua vizuri sana kuliko sisi
tunavyojua, makusudi yetu yaliyojificha moyoni mwetu, na chuki zetu
zilizojificha ndani. Lakini tunahitaji kuifunua mioyo yetu kwake yeye atujuaye
mpaka ndani kabisa, na atupendaye milele. Uponyaji unaweza kuanza Yesu anapoweza
kuyagusa majeraha yetu.
Tuombapo, Yesu, Kuhani wetu Mkuu, yu karibu nasi kutusaidia:
"Tunaye mmoja ALIYEJARIBIWA KWA KILA NJIA, KAMA SISI TUNAVYOJARIBIWA -lakini alikuwa hana dhambi. Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupate kupokea rehema na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji" - (Waebrania 4:15,16).

Je, una wasi wasi, mfadhaiko, hatia? Weka hayo mbele zake Bwana.
Ndipo yeye anaweza kukidhi kila hitaji tulilo nalo.
Je, ni lazima tuwe na mahali maalumu pa maombi hayo ya faragha?
"wewe unaposali, ingia katika chumba chako, funga mlango na kumwomba Baba yako, ambaye.. atakujazi." - Mathayo 6:6.
"wewe unaposali, ingia katika chumba chako, funga mlango na kumwomba Baba yako, ambaye.. atakujazi." - Mathayo 6:6.
Zaidi ya kuomba wakati wa kutembea mitaani, kufanya kazi, au
kufurahia mkutano fulani, kila Mkristo angekuwa na muda fulani uliotengwa kila
siku kwa maombi yake yeye peke yake pamoja na kujifunza Biblia. Tunza miadi
yako ya kila siku na Mungu wako wakati unapokuwa mchangamfu sana na wakati
unapokuwa makini sana.
4. Maombi Ya Hadhara
Kujiunga pamoja na wengine katika maombi huwaunganisha watu kwa
kifungo maalum na kukaribisha uweza wa Mungu kwa njia ya pekee.
"Kwa kuwa wawili au watatu wanapokusanyika pamoja katika
jina langu, nipo pamoja nao pale." - Mathayo 18:20.
Mojawapo ya mambo makuu kuliko yote tuwezayo kufanya sisi kama
familia ni kukuza maisha ya maombi ya pamoja. Waonyesheni watoto kwamba
tunaweza kupeleka mahitaji yetu kwake moja kwa moja. Watakuwa na msisimko juu
ya Mungu watakapoona anajibu maombi yanayohusu mambo halisi ya maisha yao.
Ifanyeni ibada ya familia kuwa wakati wa furaha na kubadilishana uzoefu wa
maisha katika hali ya uhuru.
5. Siri Saba Za Maombi Yanayojibiwa
Musa alipoomba, Bahari ya Shamu iligawanyika. Eliya alipoomba,
moto ulishuka kutoka mbinguni. Danieli alipoomba, malaika aliyafumba makanwa ya
simba wale wenye njaa kali. Biblia inatueleza visa vingi vya kusisimua vya
maombi yaliyojibiwa. Tena inapendekeza kwetu maombi kama njia ya kupata ule
uweza kwetu maombi kama njia ya kupata ule uweza mkuu wa Mungu. Yesu anaahidi
hivi:
"Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nami nitalifanya" - (Yohana 14:14).
"Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nami nitalifanya" - (Yohana 14:14).
Lakini maombi mengine bado yanaonekana kana kwamba hayasikilizwi.
Kwa nini? Hapa chini zipo kanuni saba zitakazokusaidia wewe kuomba kwa ufanisi
zaidi:
(1) Uwe karibu sana na Kristo.
"NINYI MKIKAA NDANI YANGU, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtapewa." - Yohana 15:7.
"NINYI MKIKAA NDANI YANGU, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtapewa." - Yohana 15:7.
Tunapoupa kipaumbele uhusiano wetu na Mungu na kuwa karibu naye,
tutakuwa tunasikiliza na kutazamia kupata majibu kwa maombi yetu ambayo,
vinginevyo, tusingeyatambua.
(2) Endelea Kumtumaini Mungu.
"MKIAMINI, mtapokea yote myaombayo katika sala zenu" - (Mathayo 21:22).
"MKIAMINI, mtapokea yote myaombayo katika sala zenu" - (Mathayo 21:22).
Kuamini au kuwa na imani, maana yake ni kwamba tunamtazamia Baba
yetu aliye mbinguni kwamba kweli atatupa hayo mahitaji yetu. Kama wewe una
wasiwasi kwamba huna imani, basi, kumbuka kwamba Mwokozi alitenda mwujiza kwa
mtu yule aliyemsihi sana akiwa amekata tamaa, aliyesema:"
"Naamini, nisaidie kutokuamini kwangu!" - (Marko 9:24).
"Naamini, nisaidie kutokuamini kwangu!" - (Marko 9:24).
Wewe kazana tu kuitumia imani ULIYO nayo; usiwe na waiswasi juu ya
imani ile usiyo nayo.
(3) Jisalimishe kimya kimya chini ya mapenzi ya Mungu.
"Huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu cho chote SAWA SAWA NA MAPENZI YAKE, anatusikia" - (1 Yohana 5:14).
"Huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu cho chote SAWA SAWA NA MAPENZI YAKE, anatusikia" - (1 Yohana 5:14).
Kumbuka kwamba Mungu anataka kutufundisha sisi, pamoja na kutupa
sisi vitu, kwa njia ya maombi. Kwa hiyo, wakati mwingine anatuelekeza upande
mwingine. Maombi ni njia ya kutusogeza sisi zaidi na zaidi karibu na mapenzi ya
Mungu. Hisia zetu zinatakiwa ziwe kali kutambua majibu ya Mungu na kujifunza
kitu kutokana nayo. Kuyafuatilia kwa karibu maombi yetu fulani fulani ya pekee
pamoja na kile kinachotokea kuhusiana nayo ni msaada mkubwa kwetu.
Roho Mtakatifu atakusaidia kulenga shabaha yenyewe: "Roho
anawaombea watakatifu kulingana na mapenzi ya Mungu" (Warumi 8:27. Kumbuka
kwamba mapenzi yetu yangeweza kulandana siku zote na mapenzi ya Mungu endapo
sisi tungeweza kuona kama yeye anavyoona.
(4) Mngojee Mungu kwa Saburi.
"NALIMNGOJA BWANA KWA SABURI, akaniinamia akakisikia kilio changu" - (Zaburi 40:1).
"NALIMNGOJA BWANA KWA SABURI, akaniinamia akakisikia kilio changu" - (Zaburi 40:1).
Jambo kubwa hapo ni kukaza mawazo yako yote kwa Mungu, kukaza
mawazo yako yote juu ya suluhisho lake. Wala usithubutu kumwomba Mungu
akusaidie kwa dakika moja, na halafu kujaribu kuzizamisha shida zako kwa
kujifurahisha katika anasa dakika inayofuata. Umngoje Bwana kwa saburi;
tunahitaji kuwa na nidhamu hiyo vibaya sana.
(5) Usiing'ang'anie Dhambi iwayo yote.
("Kama ningalinuia maovu moyoni, Mwenyezi-Mungu hangalinisikiliza")- Zaburi 66:18.
("Kama ningalinuia maovu moyoni, Mwenyezi-Mungu hangalinisikiliza")- Zaburi 66:18.
Dhambi ijulikanayo hukata mara moja uweza wa Mungu katika maisha
yetu; inatutenga mbali na Mungu (Isaya 59:1-2). Huwezi kuishika na
kuing'ang'ania dhambi kwa mkono mmoja na kunyosha mkono mwingine kupokea msaada
wa Mungu. Ungamo la dhambi litokalo moyoni hasa pamoja na toba ya kweli ndilo suluhisho
la tatizo hilo.
Kama sisi hatutaki kumruhusu Mungu kutuweka huru mbali na mawazo,
maneno na matendo yetu mabaya, basi, maombi yetu hayawezi kutuletea jibu lo
lote.
"Hata mwaomba, wala hampati, kwa sababu mwaomba vibaya, ili
mvitumie kwa tamaa zenu" - (Yakobo 4:3).
Mungu hatajibu "ndiyo" kwa maombi ya uchoyo. Acha wazi
masikio yako yapate kuisikia sheria ya Mungu [Amri Kumi], yaani, mapenzi yake,
naye ataacha masikio yake wazi kuzisikia dua zako.
"Yeye aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria [Amri Kumi],
hata sala yake ni chukizo" - (Mithali 28:9).
(6) Tambua Kwamba Unamhitaji Mungu.
Mungu huwajibu wale wanaoomba kuwako kwake na uweza wake katika maisha yao.
(6) Tambua Kwamba Unamhitaji Mungu.
Mungu huwajibu wale wanaoomba kuwako kwake na uweza wake katika maisha yao.
"Heri wenye njaa na kiu ya haki, maana hao
watashibishwa." - Mathayo 5:6.
(7) Kuendelea Kuomba Tu.
Yesu alitoa kielelezo cha kuwapo kwa haja ya kuendelea tu kutoa dua zetu kwa kusimulia kisa kile cha mjane aliyekuwa anaendelea tu kuomba na kuendelea kuja kwa hakimu akiwa na ombi lake lile, lile. Mwishowe yule hakimu alisema, huku akiwa ameudhika vibaya sana, "Kwa kuwa mjane huyu ananiudhi, nitahakikisha kwamba nampatia haki yake." Kisha Yesu alitoa hitimisho lake hili: "Je! Mungu hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku? Je! atazidi kuahirisha kuwapatia haki yao?" (Luka 18:5-7).

Zungumza na Mungu juu ya mahitaji yako yote, matumaini yako yote,
na ndoto zako zote. Omba mibaraka ya pekee, omba msaada unapokuwa na shida.
Endelea kutafuta, tena endelea tu kusikiliza, mpaka ujifunze kitu fulani
kutokana na jibu lake Mungu.
6. Malaika Wanayahudumia Mahitaji Ya Waombao
Mtunga Zaburi alishangilia kwamba kwa njia ya huduma ya malaika wa
Bwana maombi yake yalijibiwa:
"Nalimtafuta BWANA akanijibu; akaniponya na hofu zangu zote... malaika wa BWANA hufanya kituo kuwazunguka wale wamchao na kuwaokoa" (Zaburi 34:4-7).
"Nalimtafuta BWANA akanijibu; akaniponya na hofu zangu zote... malaika wa BWANA hufanya kituo kuwazunguka wale wamchao na kuwaokoa" (Zaburi 34:4-7).
Tunapoomba, Mungu anawatuma malaika zake kujibu maombi yetu
(Waebrania 1:14). Kila Mkristo anaye malaika wake mlinzi anayetembea pamoja
naye:
"Angalieni msimdharau mmojawapo wa wadogo hawa. Kwa maana nawaambia ya kwamba MALAIKA WAO mbinguni siku zote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni." - Mathayo 18:10.
"Angalieni msimdharau mmojawapo wa wadogo hawa. Kwa maana nawaambia ya kwamba MALAIKA WAO mbinguni siku zote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni." - Mathayo 18:10.
Kwa sababu ya maombi yetu tunayotoa:
"Bwana yu karibu. Msiwe na wasiwasi na jambo lo lote, lakini katika kila jambo kwa maombi na dua zetu pamoja na kushukuru, wekeni mambo yenu myatakayo mbele zake Mungu. Ndipo amani ya Mungu, ipitayo ufahamu wote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu." - Wafilipi 4:5-7.

7. Mtindo Wa Maisha Ya Kikristo
Biblia inaeleza wazi juu ya mtindo wa maisha ya Kikristo.
Kulingana na Waefeso 4: 22-24, Mkristo anatakiwa ku"vua" mtindo wake
wa maisha ya zamani uliotokana na "tamaa zenye kudanganya", na
ku"vaa" mtindo mpya wa maisha ambao ume"umbwa kwa mfano wa
Mungu." Katika maandiko hayo na mwongozo tuligundua kwamba wakati ule wa
kuzaliwa upya sisi tuna"umbwa upya" kuwa watu tofauti ndani ya
Kristo.
Mwongozo huu na miongozo sita inayofuata hutangaza upya mtindo wa
maisha ya Mkristo; huifunua siri ya maisha ya Kikristo yenye furaha.
Itakusaidia wewe kujenga uhusiano wenye nguvu zaidi na Kristo, ambao matokeo
yake yatakuwa mtindo wa maisha ya Kikristo ulio tofauti. Kwa hiyo kaza macho
yako kwa Yesu leo hii, nawe unaweza kuwa na sehemu katika sherehe ile ya mwisho
ya ushindi wakati amani yake Kristo itakapotawala bila kupingwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni