Swali gani hili?
Ninakusikia unauliza kama wachumba wanaweza kukaribiana kimapenzi pasipo kuangushana dhambini? Swali gani hili?! Hatukuwaambia vijana wachumbiane mbali kwa mbali ili kukimbia “tamaa za ujanani” (2 Timotheo 2:22)? Utaulizaje swali jepesi lenye jibu la wazi?
Ndiyo, huenda ninauliza jibu. Lakini nina wasiwasi na jibu lako, kwa jinsi ulivyodakia haraka. Umelipima jibu lako sawa sawa?
Ninavyofahamu mimi (kwa uzoefu wa maisha na uelewa wa Maandiko) wachumba hawakomai vya kutosha wanapokaa mbali mbali kwa kisingizio cha kukimbia “tamaa za ujanani.” Kama umepitia uchumba wa miezi sita au zaidi, utakumbuka, uchumba wenu ulikuwa kitaru cha kuwakuza kwa ajili ya ndoa. Taratibu na hatua kwa hatua upendo wenu uliwaleta pamoja mpaka mlipofika madhabahuni na kugundishwa mkiwa mmeshikanishwa mikono kama mume na mke. Mngewezaje kufikia hatua ya kupandikizwa katika ndoa kama hamkutokea kwenye kitaru?
Utakumbuka tena, afya yenu kwenye kitaru ilitabiri hali yenu katika ndoa. Mlikuwa mnaweza kuonekana pamoja hadharani, sasa hamuoni shida kukaa kiti kimoja kanisani. Mlikuwa mnaweza kushikisha breki ashiki zenu, sasa mnaweza kujizuia kutoka nje ya ndoa (usishangae, huenda vijana leo wana breki zinazoshika vizuri zaidi kuliko wanandoa walio na nidhamu ya kubakia njia kuu pasipo kuchepuka pembeni). Kama wachumba wasipokimbizwa au kukimbiana; kama watabakia huru kukaribiana na kukuza penzi lao kwa weredi na nidhamu, mbele ya Mungu na walezi na marafiki, hakika ndoa yao itasimama wima kama mininga ya milimani.
Lakini inawezekana, kweli, kwa wachumba kukuza uhusiano wao kwa ukaribu pasipo kuangushana katika “tamaa za ujanani”?
Hilo sasa ni swala la imani. Inawezekana kuonekana vigumu kwa mchumba “kusubiri” na bado kutambulika mpenzi wa karibu kama ngamia kupita tundu la sindano na bado kutambulika kama ngamia. Sawa ni vigumu. Lakini Yesu ameamua utata huo aliposema, “kwa wanadamu haiwezekani, bali kwa Mungu sivyo; maana yote yawezekana kwa Mungu” (Marko 10:27).
Nasikia kwa mbali ukiuliza: kwa vipi, yawezekanaje mambo haya? Niache sasa niongee na kijana “aaminiye” (Marko 9:23)

Huhitaji kumkimbia
Kijana mkristo, huhitaji kumkimbia mpenzi wako iii kuwa salama mbali na majaribu. Kukimbia “tamaa za ujanani” kwa miguu ni kujichosha bure. Utaenda wapi usikutane nazo? Sio faraghani tu hata hadharani vichocheo vya tamaa vipo (mwenzako mimi nakutana navyo kanisani kama ninapokutana nayo barabarani). Pote pote hadharani na faraghani vishawishi vya kukosesha vinapatikana. Kama si kwa macho, basi kwa simu na kwa televisheni na kwa mtandao na kwa mengineyo. Sawa, ole wake aletae “mambo ya kukosesha;” lakini wewe huwezi kuepuka makwazo maana “hayana budi kuja” (Mathayo 18:7). Utakimbilia wapi duniani hapa ili uwe salama?
Waumini wa Korinto walimuelewa vibaya Paulo alipowaambia wasichangamane na wazinzi (1Wakorinto 5:9). Upesi akawasahiisha kwa kuwaambia, “Sisemi msichangamane kabisa na wazinzi wa dunia hii, au na wenye kutamani,…; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia.” (1Wakorinto 5:10). Hata Yesu alipotuacha hakutuombea kwa Baba tutoke ulimwenguni uliojaa “tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima” bali alitaka tulindwe na yule mwovu (Yohana 17:15; 1Yohana 2;16).
Kando na sababu kwamba dunia haina mahali salama pa kukimbilia, ipo sababu nyingine ya kutomkimbia mchumba wako kwa kisingizio cha kukimbia “tamaa za ujanani.”

Huwezi kujikimbia
Huwezi kujikimbia. Kama unatamaa mbaya hata kama ungekimbilia mbinguni ungeishia kuwawakia tamaa malaika watakatifu.
Moto wa tamaa huanzia nafsini mwako si kwa mlengwa wako wa tamaa. Anayemsingizia mwingine kwamba amemjaribu amesahau moto ulipoanzia (Yakobo 1:13,14). “Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano” (Mathayo 15:19). Hata unapomlegezea macho ya uzinzi, unzinzi haukuanzia machoni bali moyoni. Msikie Yesu anavyosema, , “mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake” (Mathayo 5:28).
Huwezi kutazama tofauti na jicho linavyoonesha. Taa ya mwili ni jicho (Mathayo 6:22). Moyo wako ukiwa safi, badala ya kuona ukaribu wa mapenzi kama fursa ya dhambi, utaona ukaribu kama fursa ya kupendana kwa dhati. Lakini jicho lako likiwa bovu, ukaribu wowote utauona kama fursa ya kushiriki matendo ya giza. Basi, ikiwa mwanga ulioko ndani yako ni giza, basi, hilo ni giza la kutisha mno.(Mat 6:23).
Kwa maneno mengine, mtu “aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo” (Mithali 23:7). Ukiwa mpera utazaa mipera bila kujali umepandwa wapi. Mzinzi atazini kwa macho na mrembo wa barabarani; na akikubaliwa, atafanya ngono na mchumba wake faraghani.
Ikiwa kama hakuna mahali salama duniani pa kukimbilia na kama hamuwezi kukimbia mioyo yenu ya tamaa, mfanyeje ili muendeshe mapenzi ya dhati na salama?
Huna la kufanya zaidi ya kusalimisha mioyo yenu kwake “Yeye awezaye kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu; Yeye aliye Mungu pekee, Mwokozi wetu kwa Yesu Kristo Bwana wetu;...” (Yuda 24,25) . Unaonesha bidii kuchunga sana moyo wake kuliko vyote ulindavyo (Mithali 4:23) unapojisalimisha ndani ya mikono ya Mungu inayotoa ulinzi wa masaa 24 na kwa siku 7 mfululizo.

Mungu atawalinda
Wewe na mwenzako, mnadhamiria kweli kutunza mioyo yenu na uchumba wenu mikononi mwa Mungu mpaka Mchungaji atakapowatangaza mmekuwa mume na mke? Kama ndivyo, nawapongeza na nawaambia inawezekana; kwa Mungu yote yawezekana (Luka 18:27). Kwa sababu Mungu “ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.” (2Pet 1:4).
Mungu anawafanya washirika wa tabia yake kwa kuwapa fikra mpya. Kwa uwezo wa Roho wake, atawawezesha mtazamane tofauti na media inavyowaelekeza. Utajitambua na kumtambua mwenzio kama Mungu anavyowatambua. Ni kwa mtazamo huo mpya na msaada wa Roho mtaweza kuvipita vikwazo vya uaminifu pasipo mawaa katika furaha kuu. Kubarini basi kufanywa “wapya katika roho ya nia zenu” (Waefeso 4:23)
Upya huo wa fikra na roho na nia si sawa na wa kidunia. Ulimwengu unatangaza kwamba mapenzi ni ngono na ngono ni mapenzi. Mabango ya ujumbe wake yameandikwa kwa herufi kubwa kwa ubongo wako kuusoma pasipo wewe kuwa na habari.
Biblia nayo inahubiri kinyume chake ikisisitiza: mapenzi ni zaidi ya ngono na keki ni zaidi ya sukari. Zaidi ya hisia tamu, mapenzi ya kweli ni uchaguzi wa wapendanao kujitoa kupendana na kufurahiana. Kama Kristo alivyojitoa kwa furaha kwa bibi arusi wake, ndivyo mpenzi anavyopaswa kujitoa kwa hiari kwa mwenzake (Waefeso 5:22,25). Unahitaji kiriba kipya kwa divai mpya (Mathayo 9:17) na kichwa kipya kwa mafundisho haya mpya. Hamuwezi kuchanganya nadharia ya kibiblia ya upendo na uelewa wa kidunia wa mapenzi. Fanyweni “wapya katika roho ya nia zenu.”
Upendo wa kujitoa uliosifiwa vizuri sana katika Wakorinto 13 mnaweza kuuthamini mkichukua mtazamo mpya. Someni sura hiyo pamoja. Rudieni tena na tena. Tafakarini pamoja maneno yake. Ruhusuni mwangaza wa dhahabu toka kurasa takatifu umulike bongo zenu mpaka propaganda potovu zipoteza mvuto machoni penu.
Maneno ya Paulo aliyowaandikia wakolosai yasitoroke macho yenu. Aliwaambia wavue utu wao wa kale wa kupendana kwa kudanganyana na badala yake wavae “utu mpya, unaofanywa upya…sawasawa na mfano wake yeye aliyeuumba” (3:9, 10). Mnapotambua Yesu na si ngono inayowaunganisha wapenzi mtakuwa mmejiokotea lulu ya thamani kubwa. Hamtasita kuuza nadharia nyingine zote pinzani ili kuikamata elimu hii bila kuiachia.
Unataka kujua uchumba wenu utachukua sura gani mnapofanywa upya?
Mapenzi ya dhati katika picha
Tazama jinsi ilivyo vema na kupendeza kuwaona wachumba waliozaliwa upya wakipendana. Badala ya kushikamana kwa pingu za ngono sasa wamefunguliwa na kuachwa huru kupendana kwa hiari. Huwasikii tena wakisema, “nimezidiwa na tamaa; nisaidie mara hii tu.” Kwa sababu, hawaburuzwi na ashiki; hawasukumwi na tamaa; bali wanaongozwa na Roho (Warumi 8:5). Watazame tena. Huwasikii wavulana wanaojua uhuru wakisema “usiponipa….basi hunipendi.” Hawashiki mashati wapenzi wao na hawawadai upendo. Maana wanatawaliwa na upendo ambao “hautafuti mambo yake” (1Wakorinto 13:5). Tena huwasikii wasichana waliofunguliwa wakisema “hebu nimpe… ili anipende”. Hawasukumwi na hofu katika kupenda; maana, “mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo” (1Yohana 4:18). Waumini wa kweli ndiyo wanaojua kupenda kwa kweli.
Tofauti na wapenzi wa kutekana na kuburutana na kuchukuana wakiwa na vitambaa vyeusi machoni, wapenzi waliofanywa huru na Mwana (Yohana 8:36) wako huru kweli kweli kutoa na kupokea upendo. Huo ndiyo uhuru wa kweli ambao mipaka yake inapaswa kulindwa kwa gharama zote. Hakuna serikali chini ya jua inayothamini uhuru isiyolinda mipaka yake. Hakuna wapenzi walioelimika kupendana kwa dhati wanaojiachia kuingiliana isivyopaswa. Injili ni kinga ya utumwa wa mapenzi haramu.
Ufahamu wa injili unapowalinda wapendanao, inawaacha huru kufahamiana kwa ukaribu ndani ya wigo wake. Huku wakijihesabu kila mmoja ni kiungo cha mwenzake, wapenzi waliofunguliwa wanajisikia huru kuuvua uongo na kujifunza kusema ”kweli kila mtu na jirani yake” (Waefeso 4:25). Mioyo yao huachwa wazi kutazamwa mpaka uvunguni; hawana siri za kuzificha. Wanajiachia wanapoongea; hawana breki za kuzishika. Wanajieleza pasipo kukoboa maneno; hawahangaiki na maandalizi kabla ya kuongea. Wako huru kucheka mpaka jino la mwisho; hawana hofu ya kujiachia. Hawajilindi nyuma ya ngozi kwa tabasamu za kupachika. Hawaigizi. Wana Yesu ndani-nje. Kila mmoja wao anafurahia kujitupia jumla jumla mikononi mwa mwenzake pasipo hofu ya kuangushana. Pendo lao “hufurahi pamoja na kweli” (1 Wakorintho 13:6).
Mwisho lakini sio mwisho
Mpaka hapo, unaweza kuuliza: wapi upendo wa aina hiyo umefanyika mwili nasi tuweze kuunyoshea kidole hata kusema huu hapa? Twende Paris au Zanzibar au wapi tukutane na mapenzi yasiyoigizwa na yanayofaa kuigwa? Usikae mbali. Nitarudi tena nikuoneshe.

WAKO
INJILI KWA KILA NYUMBA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni