JE, UNAIFAHAMU MAANA YA INJILI YA KWELI AU UNAHUBIRI TU? TAHADHARI! Wagalatia 1:1-9
Wagalatia 1: 8; Neno linasema:-“ Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe. 9 Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe.”
1. Maana ya injili – ni habari njema sana!
• Kwa kiyunani (kigiriki) ni Evangelion, kwa Kilatini ni Evangelium; na kwa Kiingereza ni Gospel (God Spell, spell=tangazo/mahubiri kwa makusudi ya kuleta au kusababisha tukio maalumu). Zipo habari njema za namna mbali mbali kulingana na nini kinaonekana ni kitu chema kinachohubiriwa katika habari njema hiyo. Zipo habari njema za namna nyingi – INJILI ZA NAMNA NYINGINE NYINGI! Lakini sisi na ulimwengu wote siku za leo TUNAHITAJI INJILI YA KWELI KUTOKA KWA MUNGU WA KWELI ALIYE HAI MILELE NA MILELE! Kwa maana HAKUNA MWEMA, ILA MUNGU PEKE YAKE!
2. Sababu za kujifunza somo hili:
a. Ili tuweze kuifahamu maana ya injili – INJILI YA KWELI! Wahubiri na wakristo wengi kwa sababu ya kutoelewa maana ya kweli ya injili ya Wokovu wamepata shida ya kuichanganya injili ya kweli na
i. Mafanikio na Baraka za kimwili katika maisha ya dunia hii
ii. Siasa na umaarufu wa kidunia
iii. Burudani, starehe, na makusanyiko ya kidunia.
iv. Dini na madhehebu; dini mpya?
v. Kuchanganyikiwa na kudanganyika?
b. Ili tuweze kujua ni nini KIINI KIKUU CHA INJILI YA KWELI.
i. Wengine hufikiria ya kuwa kiini cha injili ya kweli ni :-
1. Dini – au dini mpya
2. Siasa au chama
3. Baraka, miujiza, uponyaji, mali na mafanikio ya kidunia – kuirithi nchi milele?
4. Pesa, mali, utajiri, mke/mume,?
c. Ili tujue sifa, tabia, na matokeo ya injili ya kweli ni nini?
i. Uweze kuepukana na hali ya kuigeukia ijili nyingine kama mkristo au kanisa zima.
ii. Usije ukashiriki kuihubiri injili nyingine na mafundisho ya mashetani na kupata laana!
3. TUNAHITAJI INJILI YA KWELI KUTOKA KWA MUNGU WA KWELI ALIYE HAI MILELE NA MILELE! Kwa maana HAKUNA MWEMA, ILA MUNGU PEKE YAKE! INJILI HIYO NI:
a. Nini maana ya injili ya kweli? Ni injili yake BWANA YESU KRISTO WA NAZARETH, ni habari zake BWANA YESU KRISTO MWANA WA MUNGU ALIYE HAI. Tunasoma katika Matendo ya Mitume 10: 34 Petro akafumbua kinywa chake, akasema, Hakika natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo; 35 bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye. 36 Neno lile alilowapelekea wana wa Israeli akihubiri habari njema ya amani kwa Yesu Kristo (ndiye Bwana wa wote), 37 jambo lile ninyi mmelijua, lililoenea katika Uyahudi wote likianzia Galilaya, baada ya ubatizo aliouhubiri Yohana; 38 habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye. 39 Nasi tu mashahidi wa mambo yote aliyoyatenda katika nchi ya Wayahudi na katika Yerusalemu; ambaye walimwua wakamtundika mtini. 40 Huyo Mungu alimfufua siku ya tatu, akamjalia kudhihirika, 41 si kwa watu wote, bali kwa mashahidi waliokuwa wamekwisha kuchaguliwa na Mungu, ndio sisi, tuliokula na kunywa pamoja naye baada ya kufufuka kwake kutoka kwa wafu. 42 Akatuagiza tuwahubiri watu na kushuhudia ya kuwa huyu ndiye aliyeamriwa na Mungu awe Mhukumu wa walio hai na wafu. 43 Huyo manabii wote humshuhudia, ya kwamba kwa jina lake kila amwaminiye atapata ondoleo la dhambi. 44 Petro alipokuwa akisema maneno hayo Roho Mtakatifu akawashukia wote waliolisikia lile neno.
b. NI NINI KIINI KIKUU CHA INJILI YA KWELI? Ni BWANA YESU KRISTO WA NAZARETHI, MWANA WA MUNGU ALIYE HAI MILELE NA MILELE!
i. Tunasoma katika Matendo ya Mitume 8:4 Lakini wale waliotawanyika wakaenda huko na huko wakilihubiri neno. 5 Filipo akatelemka akaingia mji wa Samaria, AKAWAHUBIRI KRISTO.
ii. Na katika Warumi 1:1 Paulo, mtumwa wa Kristo Yesu, aliyeitwa kuwa mtume, na kutengwa aihubiri Injili ya Mungu; 2 ambayo Mungu amekwisha kuiahidi kwa kinywa cha manabii wake katika maandiko matakatifu; 3 YAANI, HABARI ZA MWANAWE, ALIYEZALIWA KATIKA UKOO WA DAUDI KWA JINSI YA MWILI, 4 NA KUDHIHIRISHWA KWA UWEZA KUWA MWANA WA MUNGU, KWA JINSI YA ROHO YA UTAKATIFU, KWA UFUFUO WA WAFU, YESU KRISTO BWANA WETU; 5 ambaye katika yeye tulipokea neema na utume ili mataifa yote wapate kujitiisha kwa imani, kwa ajili ya jina lake; 6 ambao katika hao ninyi mmekuwa wateule wa Yesu Kristo;
iii. INJILI NYINGINE ISIYO YA KWELI- ni injili asiyohubiriwa BWANA YESU KRISTO, hata kama muhubiri au wanasema habari za Mungu kwa kutumia Biblia – hiyo ni injili nyingine, jihadhari! Tunaona hatari hii katika Matendo ya Mitume 8: 9 Na mtu mmoja, jina lake Simoni, hapo kwanza alikuwa akifanya uchawi katika mji ule, akiwashangaza watu wa taifa la Wasamaria, akisema ya kuwa yeye ni mtu mkubwa. 10 Wote wakamsikiliza tangu mdogo hata mkubwa, wakisema, Mtu huyu ni uweza wa Mungu, ule Mkuu. 11 Wakamsikiliza, kwa maana amewashangaza muda mwingi kwa uchawi wake. 12 Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake. 13 Na yeye Simoni mwenyewe aliamini akabatizwa, akashikamana na Filipo; akashangaa alipoziona ishara na miujiza mikubwa inayotendeka. 14 Na mitume waliokuwako Yerusalemu, waliposikia ya kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu, wakawapelekea Petro na Yohana; 15 ambao waliposhuka, wakawaombea wampokee Roho Mtakatifu; 16 kwa maana bado hajawashukia hata mmoja wao, ila wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu.
iv. JAPOKUWA ALISEMA ANAHUBIRI HABARI ZA MUNGU MKUU, LAKINI KIINI CHA INJILI YAKE KILIKUWA YEYE MTUMISHI(SIMON) NI MTU MKUBWA!(Soma mstari wa 9)17 Ndipo wakaweka mikono yao juu yao, nao wakampokea Roho Mtakatifu. 18 Hata Simoni alipoona ya kuwa watu wanapewa Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono ya mitume, akataka kuwapa fedha akisema,
19 Nipeni na mimi uwezo huu, ili kila mtu nitakayemweka mikono yangu, apokee Roho Mtakatifu. 20 Lakini Petro akamwambia, Fedha yako na ipotelee mbali pamoja nawe, kwa kuwa umedhania ya kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali. 21 Huna fungu wala huna sehemu katika jambo hili, kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele za Mungu. 22 Basi, tubia uovu wako huu, ukamwombe Bwana, ili kama yamkini, usamehewe fikira hii ya moyo wako. 23 Kwa maana nakuona u katika uchungu kama nyongo, na tena u katika kifungo cha uovu. 24 Simoni akajibu, akasema, Niombeeni ninyi kwa Bwana, yasinifikilie mambo haya mliyosema hata moja.
v. TOFAUTI NA FILIPO ALIYEHUBIRI INJILI YA KWELI! Tunasoma Matendo ya Mitume 8:4 Lakini wale waliotawanyika wakaenda huko na huko wakilihubiri neno. 5 FILIPO AKATELEMKA AKAINGIA MJI WA SAMARIA, AKAWAHUBIRI KRISTO.
c. Sifa, tabia, na matokeo ya Injili ya kweli ni nini?
i. Kiini chake kikuu ni BWANA YESU KRISTO – tunasoma katika Luka 2:8-20; Matendo ya Mitume 8:4-5.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni