Napenda
kuanza kukuambia ya kuwa si mapenzi ya Mungu uwe maskini. Kwa sababu
tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu huu, Mungu hakupanga kuwa watu wake
aliowaumba wawe maskini; bila kujali rangi, kabila, wala taifa.
Nafahamu ya kuwa katika Mathayo 5:3, Yesu Kristo alisema; “Heri
walio maskini wa roho; maana ufalme wa mbinguni ni wao.” Watu wengi
wanapousoma mstari huu, wanadhani Yesu Kristo alisema “Heri walio
maskini wa mahitaji ya MWILI; maana ufalme wa mbinguni ni wao.” Lakini
Kristo hakusema hivyo.
Mtu maskini maana yake ni mtu
mhitaji. Yesu Kristo aliposema “Heri walio maskini wa roho …….”Alikuwa
ana maana ya kusema ‘Heri walio wahitaji wa mambo ya rohoni; maana
ufalme wa mbinguni ni wao. Ndiyo maana aliongeza kusema, “Heri wenye
njaa na kiu ya haki; maana hao watashibishwa"(Mathayo 5:6).
Mtu aliye maskini wa mambo ya mwili ni yule aliye mhitaji wa
mambo ya mwili. Na mambo ya mwilini ninayoyasema ni mavazi, chakula na
mahali pa kulala. Yesu Kristo hakusema heri wale walio na mahitaji ya
chakula, mavazi, afya na malazi.
Ninaposema mahitaji ya
mwili usije ukachanganya na matendo ya mwili yaliyoandikwa katika
Wagalatia 5:19-21 ambayo ni uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu,
uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda na
ulevi. Mimi siyazungumzii hayo ninaposema juu ya mahitaji ya mwili.
Mahitaji ya mwili ninayoyasema ni mavazi, chakula, nyumba na matibabu.
Kwa hiyo si sawa kabisa kwa mtu kuhalalisha umaskini wa mwili,
yaani ukosefu wa chakula, mavazi, matibabu na nyumba, kwa kutumia maneno
ya Bwana Yesu Kristo yaliyo katika Mathayo 5:3:
Nataka kurudia tena; si mapenzi ya Mungu mtu awe maskini.
Unaweza ukaniuliza na kusema, “Bwana Mwakasege kama si mapenzi ya
Mungu mtu awe maskini, mbona basi kuna matajiri na maskini, je! Mungu
hakuwaumba wote?
Ni kweli kwani hata imeandikwa katika
Mithali 22:2, kuwa “Tajiri na maskini hukutana pamoja; Bwana ndiye
aliyewaumba wote”. Lakini fahamu ya kuwa ingawa matajiri na maskini
waliopo wote waliumbwa na Mungu; tangu mwanzo wa uumbaji Mungu
hakuyaweka matabaka haya mawili.
Hapo mwanzo Mungu
alipomuumba mtu, hakuweka ndani yake utajiri na umaskini pamoja. Wala
hakuumba watu wengine wawe matajiri na wengine wawe maskini.
Tunafahamu ya kuwa mtu aliumbwa kwa mfano wa Mungu na kwa sura ya
Mungu. Na naamini ya kuwa utakubaliana nami nikisema Mungu wetu si
maskini kwa hiyo hatukuumbwa kwa mfano wa kimaskini wala sura ya
kimaskini.
Kwa nini nasema na kusisitiza ya kuwa si mapenzi ya Mungu tuwe maskini?
Ninazo sababu nne ambazo ningependa kukushirikisha:
Mungu ndiye atupaye nguvu za kupata utajiri
“
Bali utamkumbuka Bwana , Mungu wako, maana ndiye akupaye NGUVU ZA
KUPATA UTAJIRI; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama
hivi leo” (Kumb. 8:18).
Si mapenzi ya Mungu tuwe
maskini kwa kuwa yeye mwenyewe ndiye atupaye nguvu ili tupate utajiri!
Kama basi Mungu anatupa nguvu za kupata utajiri, ina maana ni wazi
kwamba Mungu hapendi tuwe maskini wa mambo ya mwilini.
Lakini fahamu ya kuwa si matajiri wote waliopo duniani wameupata utajiri
kutokana na nguvu walizopewa na Mungu. Wengi wamepata utajiri kwa njia
ya dhuluma. Na ndiyo maana sehemu nyingi katika Biblia matajiri wa jinsi
hiyo wamekemewa. Soma Amosi 5:11, 12. Kwa sababu hii Mungu hayuko
upande wa matajiri hawa. Hii pia haimaanishi kuwa Mungu yuko upande wa
KILA maskini aliopo duniani. La hasha! Mungu yuko upande wa yule
ayafanyaye mapenzi yake awe tajiri au maskini (Mathayo 7:21)
Watu wengi wametajirika kwa njia ya rushwa na kutokusimamia haki
pamoja na uchoyo. Na hii si sawa hata mbele za Mungu. Ni dhambi zilizo
wazi kabisa. Na wote wafanyayo hayo wanahitaji kutubu!
Ngoja nikueleze jambo muhimu: Mungu anapokupa nguvu za kupata utajiri, anakupa akiwa na lengo na kusudi muhimu.
Ni lengo gani hilo?
Imeandikwa, “………. Ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo”
Na Yesu Kristo alisema, “ ……. Kikombe hiki ni AGANO JIPYA KATIKA DAMU YANGU, inayomwagika kwa ajili yenu” (Luka 22:20).
Mungu akikupa nguvu za kupata utajiri ni kwa ajili ya
kulifanya imara agano lake katika damu ya Yesu Kristo. Na hii ina maana
utajiri utakaokuwa nao kutoka kwa Mungu ni kwa kueneza injili! Ni kwa
ajili ya kueneza habari njema ya ukombozi kutokana na dhambi, mauti,
magonjwa na umaskini. Habari njema hii inatakiwa kuenezwa kwa maneno na
kwa matendo.
Kwa kuwa tu kuna matajiri wasio wa haki basi
haimaanishi kuwa matajiri wa haki hawapo. Ni budi tuweze kutofautisha
utajiri ulio wa haki na utajiri usio wa haki.
Mungu ndiye atufundishaye kupata faida
Mungu wetu tunayemwabudu na kumtumikia katika Kristo Yesu si Mungu wa hasara bali Mungu wa faida. Imeandikwa hivi;
“ Bwana, Mkombozi wako, Mtakatifu wa Israeli, asema hivi;Mimi ni
Bwana, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye
katika njia ikupasayo kuifuata”(Isaya 48:17).
Ndiyo
maana kila mtu ndani yake ameumbiwa kupenda kufundishwa ili apate faida
katika mambo anayoyafanya. Mungu akikufundisha kupata faida; njia
utakayotumia kupata faida itakuwa njia ya haki. Na faida hiyo haitakuwa
kwa ajili yako mwenyewe, bali utawashirikisha na wengine pia faida hiyo .
Watu wengine kwa kutokuwa wavumilivu, na kutokujali mafundisho
ya Mungu; wameamua kujipatia faida kwa kuwadhulumu, kuwakandamiza na
kuwanyonya wengine. Na inasikitisha jinsi wanavyomshirikisha Mungu
katika faida najisi namna hiyo waposema ya kuwa ni Mungu aliyewasaidia
‘kudhulumu na kunyonya’. Ni wazi ya kuwa Mungu hakuwasaidia kupata faida
kwa njia ya udhalimu.
Si mapenzi ya Mungu tuwe maskini,
ndiyo maana anatufundisha ili tupate faida ya halali. Kwa ajili hiyo
imeandikwa; “Mwibaji asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akitenda
kazi iliyo nzuri kwa mikono yake mwenyewe, apate kuwa na kitu cha
kumgawia mhitaji” (Waefeso 4:28).
Je! Si jambo la kushukuru hili, la kuwa na Mungu ambaye hapendi tupate hasara?
Kama Mungu asingekuwa anapenda tufanikiwe katika mahitaji yetu ya
mwili, basi ingeandikwa wazi katika Biblia. Lakini badala yake naona
maneno kama yafuatavyo; “Mpenzi, naomba ufanikiwe katika mambo YOTE na
kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo” (3Yohana 1:2).
Kwa maneno mengine anatuombea ya kuwa kwa kadri roho
inavyofanikiwa basi tufanikiwe vivyo hivyo katika mahitaji ya mwili –
yaani tuwe na chakula, mavazi, n.k.
Vitu vyote vyema ni mali ya Bwana, na vyote vya Bwana ni vyetu ndani ya Kristo
Katika Zaburi 24:1 imeandikwa;“Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana; Dunia na wote wakaao ndani yake”
Na pia ukisoma katika Hagai 2:8 unaona imeandikwa hivi
“Fedha ni mali yangu, na dhahabu ni mali yangu, asema Bwana wa majeshi”
Ngoja nikuulize swali; Je! unadhani vitu vyote hivi Bwana
amemwekea nani? Unadhani alimwekea shetani na watu wanyonyaji wachache?
La hasha!
Mungu aliviweka vitu hvi vyote na mali hii yote kwa ajili ya
watu wake wote, ili itumike katika usawa. Kwa nini? Kwa kuwa Mungu
hapendi watu wake wawe maskini. Ndiyo maana mtu alipoumbwa aliwekwa awe
wakili wa mali yote ya Mungu hapa duniani.
Utajiri
uliomo duniani umetawaliwa na watu wachache na nchi chache siku hizi kwa
sababu ya dhambi za uchoyo, ubinafsi, uonevu,unyonyaji, unyang’anyi na
dhuluma zilizoingia ndani ya mwanadamu.
Na hii imefanya
watu wengine kufikiri ya kuwa Mungu ndiye aliyegawa matabaka haya
mawili, ambavyo si kweli. Na si vizuri kumsingizia Mungu katika jambo
ambalo mwanadamu mwenyewe amejiletea uharibufu.
Yesu Kristo alikuwa maskini ili sisi tuwe matajiri
“ Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi
alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba
ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake” (2 Wakorintho 8:9).
Je! unafahamu kwa nini Yesu Kristo aliamua kuwa
maskini? Ni “…….. ili kwamba ninyi mpate kuwa MATAJIRI kwa umaskini
wake”.
Najua kuna wengine watashangaa kuusoma mstari huu; lakini ndivyo ilivyo.
Nimewahi kusikia mkristo mmoja akisema: “ Mimi ni maskini kwa kuwa Yesu Kristo alikuwa maskini”.
Na mwingine alisema; “ Napenda kuwa maskini kwa kuwa Yesu Kristo alikuwa maskini”.
Nadhani kuwa kuna wakristo wengi ambao wana mawazo kama haya.
Ni kweli kwamba Yesu Kristo alipokuwa hapa duniani alikuwa maskini.
Lakini hakuwa maskini ili sisi tuwe maskini; bali alikuwa maskini ili
sisi tuwe matajiri! Kama alikuwa maskini ili sisi tuwe maskini kama
wengine wanavyodhani, basi kazi hiyo haina faida kwetu. Lakini Yesu
Kristo asifiwe kwa kuwa alikuwa maskini ili sisi tuwe MATAJIRI.
Na ndiyo maana alisema katika Luka 4:18a ya kuwa; “Roho wa Bwana
yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri MASKINI habari
njema.”
Je! kuna habari njema kwa maskini zaidi ya kumwondoa katika umaskini wake?
Injili ni habari njema. Na injili ni uweza wa Mungu uuletao
wokovu kwa kila aaminiye (Warumi 1:16). Kuokoka si kuenda tu mbinguni;
bali kuokoka maana yake ni uokolewe usiende motoni bali uende mbinguni
ukifa, PAMOJA na kuokolewa kutoka kwenye matatizo ukiwa hapa duniani
ambayo ni pamoja na umaskini.
Petro aliposema “Bwana
niokoe” alipokuwa anazama katika maji unafikiri alikuwa anataka wakati
huo aokoke aende mbinguni? La hasha! Yeye Petro alitaka aokoke ASIZAME
KATIKA MAJI. Na Yesu akasikia kilio chake akamwokoa. Hivi leo kuna watu
wengi mijini na vijijini wanalia Yesu awaokoe kutokana na njaa, kukosa
mavazi, magonjwa, maonezi, nakadhalika. Kanisa kama mwili wa Kristo
linatakiwa kuwa mstari wa mbele kuwasaidia watu hao, kwa kuwa kazi hii
ni sehemu ya utume wake.
Wakristo wengine utawasikia
wakisema; hapa duniani hawahitaji kitu bali thawabu yao wataipata
mbinguni. Lakini matamshi ya namna hii yanaeleza ukweli nusu na
usiokamilika. Kuwa mkristo kuna thawabu duniani na kuna thawabu
mbinguni.
Kama hakuna thawabu yoyote tunayoipata tukiwa
hapa duniani kwa kumfuata Yesu Kristo; basi ukristo wetu hauna maana na
hauna msaada wowote kwa mwanadamu. Ukristo usiotatua matatizo ya
mwanadamu ya kila siku, ni ukristo usio na uhai.
Mtume Petro naye aliwahi kusumbuliwa sana na jambo hili, hata ikabidi amuulize Bwana Yesu.
“Ndipo Petro akajibu, akamwambia, tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata, TUTAPATA NINI BASI?” (Mathayo 19:27)
“Yesu akasema, Amini, nawaambiaeni, hakuna mtu aliyeacha
nyumba, au ndugu waume, au ndugu wake, au mama, au baba, au watoto, au
mashamba, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili, ila atapewa MARA MIA
SASA WAKATI HUU, nyumba, na ndugu waume, na ndugu wake, na mama, na
watoto, na mashamba, pamoja na udhia; na katika ulimwengu ujao uzima wa
milele” (Marko 10:29,30).
Majibu haya ya Bwana Yesu,
yanazidi kutudhihirishia ya kwamba si mapenzi ya Mungu tuwe maskini.
Yesu Kristo ameeleza wazi kabisa ya kuwa atakayemwamini na kufuata
maagizo hayo atapata MARA MIA SASA WAKATI HUU akiwa bado duniani. Na
kati ya vitu atakavyopewa ni pamoja na nyumba na mashamba!
Ni kweli Bwana Yesu Kristo alipokuwa hapa duniani alikuwa maskini,
lakini baada ya kufufuka alirudishiwa utajiri wake. Ndiyo maana Mtume
Paulo anazungumzia juu ya “….. utajiri wake Kristo usiopimika”. (Waefeso
3:8). Na katika Wafilipi 4:19 tunasoma hivi; “Na Mungu wangu
atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadri ya utajiri wake, katika
utukufu, ndani ya Kristo Yesu”.
Kumbuka ya kuwa; Yesu
Kristo alichukua dhambi zetu na magonjwa yetu , na kwa kupigwa kwake
sisi tumepona (Isaya 53:5; Mathayo 8:16,17; 1Petro 2:24). Na kwa kujua
hili kanisa linajihusisha na kuombea wagonjwa na kutoa huduma za afya
kwa wagonjwa.
Kumbuka ya kuwa; Yesu Kristo alichukua
dhambi zetu na akafanyika dhambi kwa ajili yetu, “ Ili sisi tupate kuwa
haki ya Mungu katika Yeye” (2Wakorintho 5:21). Na kwa kujua hili kanisa
linahubiri habari za ondoleo la dhambi kwa yeyote atakayemwamini Kristo.
Kumbuka ya kuwa; Yesu Kristo alikuwa maskini, ingawa
alikuwa tajiri, ili kwa umaskini wake sisi tupate kuwa matajiri (2
Wakorintho 8:9). Na kwa kujua hili kanisa linajihusisha na miradi
mbalimbali ya kimaendeleo ili mtu aondokane na umaskini.
By Hezron Mwanafunzi Wa Yesu
Alhamisi, 9 Aprili 2015
KWA NINI SI MAPENZI YA MUNGU TUWE MASKINI?
About Director Hezron Marwa
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Maoni 2 :
Ninamshukuru sana Dk dawn acuna, aliandika uchawi wa mapenzi ambao ulimrudisha mpenzi wangu wa zamani katika masaa 48, shukrani kwake, ikiwa una hali kama hiyo.
*Ukitaka kumrudisha mpenzi wako.
*Kama unataka kupata mimba.
*Ukitaka kuacha kuharibika kwa mimba.
Ikiwa unataka kuponya aina yoyote ya ugonjwa. Na wengine,
Wasiliana naye yeye ndiye mtu sahihi wa kutatua tatizo hili.
Barua pepe: { dawnacuna314@gmail.com }
Whatsapp: +2348032246310
Kwa zaidi ya miaka 13 ya ndoa sikuweza kuzaa, naendelea kuharibika hata nikipata mimba, madaktari wote hawakuweza kunisaidia, hadi dada yangu akanielekeza kwa Dr DAWN, ambaye alinisaidia nikapata ujauzito na sasa hivi kuwa na mtoto mzuri wa kike,
Anasaidia pia marafiki zangu wengi niliowaelekeza, Dr DAWN ni baraka kwa kila mtu anayewasiliana naye,
*Kama unataka kupata mimba.
*Ukitaka kuacha kuharibika kwa mimba.
*Ukitaka kumrudisha mpenzi wako.
*Kama unataka mume/mkeo arudishwe.
*Kama unataka kurejesha mali yako iliyoibiwa au Pesa.
*Ukitaka kutibu aina yoyote ya ugonjwa,
Wasiliana naye kwa WhatsApp: +2349046229159
Chapisha Maoni