Fuatilia thread hii ili kupata updates za kinachojiri...
Kituo cha mabasi Ubungo
Juu hapo ni Kituo cha Mabasi - Nyegezi, Mwanza
Hapa ni Mbezi, Mabasi ya UDA Yalikuja kutoa msaada lakini yamezuiliwa kupakia abiria hivyo milango imefungwa.
=> Mtwara Magari hayakutoka kwenda Dar kwasababu hawajui hatms ya huko Dar ila walikuwa tayari kusafieisha abiria, daladala na magari ya wilayani hakuna.
=> Kuna magari yamezuiwa Chalinze, wamepewa taarifa kuwa waliotangulia mbele Chalinze wamepigwa mawe.
=> Hapa stendi ya Njombe mabasi hayajaondoka mpaka muda huu.
=> Za asubuhi, hapa stand ya Njombe mabasi hayajaondoka hadi muda huu
=> Kuna zaidi ya mabasi zaidi ya 15 kutoka kanda ya ziwa, yamezuiwa/yamekwama Wilaya ya Kibaha, wamepewa taarifa kuwa waliotangulia mbele ya Chalinze wamepigwa mawe. Wanahofia Vurugu zinazo endelea Dar es Salaam
=> Hapa Tabora, mabasi ya kwenda mikoani mpaka sasa abiria hawajui mustakabali wa safari
=> Mtwara magari hayakutoka kwenda Dar kwasababu hawajui hatma ya huko Dsm ila walikuwa tayari,daladala na magar ya wilayani hakuna
=> Hapa Mbagala Rangi 3, kuna baadhi ya daladala zimeamua kuendelea kuchukua abiria lkn zinavamiwa na madereva wanaoshinikiza mgomo. Wanawashusha abiria toka kwenye daladala
Maoni 1 :
By kivyako
Niko kituoni hapa mitaa ya Segerea, hakuna gari hata moja abiria tumeduwaa kituoni! Jinsi ya kufika kibaruani haieleweki! Je, huko ulipo hali ikoje?
By wokitoki
Wana JF leo ni majanga, nipo kituoni Mbez tangu saa kumi na moja asubuh sijapata usafiri hadi sasa, watu ni wengi mno na wengine wameamua kurud majumbani mwao baada ya kuona hamna dalili ya kupata usafir. Naskia kuna mgomo wa madereva nchi nzima.
Rai yangu kwa wahusika chondechonde wakae pamoja wamalize tofauti zao ili mgomo uishe la sivyo ni majanga makubwa.
Nawasilisha.
By Sir Good
Serikali kupitia Sumatra imekuja na kanuni mpya ya kuwataka madereva kwenda kusoma kila baada ya miaka mitatu, hii inahusu madaraja yote kuanzia A mpaka C. Ada ya kusoma kwenye vyuo vya udereva ni tsh 500,000. Mgomo huo unatokana name kupinga ujinga huo ulioletwa na serikali, hats sisi madereva wa pick up Leo Leo tumegoma! Kama mambo yatakwenda kama yalivyopangwa, lengo Leo kisitembee chombo chochote barabarani kuanzia gari, bajaji mpaka bodaboda kwani maumivu ya hiyo sheria yanatugusa wote.
By Pendael24
Abiria wana pata shida ya ajabu Morogoro, bodaboda ndio zinatoa msaada ila kwa wale wenye uwezo. Wale wenzangu na mie wapo vutuoni hawana lile wala hili, sijui migomo hii ni mpaka lini, Abood Ndio Wakati Wako Wakutoa Msaada Sasa Sio Kwenye Kuzika Tu.
By Baba Ilhaam
Hali ni tete kwa usafiri leo DSM!! Imenibidi nichukue bajaji toka simu 2OOO/Sinza mpaka maeneo ya posta!!
Hali ni mbaya
By kababaa1
Wakuu hadi saa hizi hakuna basi hata moja lililoondoka kwenda mikoani kutokea hapa Kahama.
Chapisha Maoni