Alhamisi, 14 Mei 2015

IJUE IBADA YA SIFA NA NGUVU IYOKO KATIKA SIFA

Emmanuel Kamalamo
Bwana Yesu asifiwe!
Ubarikiwe wewe upendaye kujifunza Neno la
Mungu.Na Mungu kawaweka watumishi mbalimbali
kwa mafundisho mbalimbali lengo ni kujenga kanisa
na wale ambao hajaokoka waokolewe...oh! Haleluya
glory to God!
Hakuna asiyejua maana ya SIFA.Maana tunamsifu
Mungu makanisani mwetu kila ifanyikapo ibada.
Lakini tunaweza tukamsifu Mungu ndani ya ibada
lakini sifa zisimfikie Mungu...Najua utauliza kwa
nini?
Nisikilize si kila wimbo ni wa sifa mbele za BWANA.
Mfano wimbo huu"MWAMBIE FARAO NIMEOKOKA
SITARUDI TENA MISRI NAELEKEA KANAANI" au "
KANYAGA SHETANI KANYAGA" Si kwamba nyimbo
hizi ni mbaya na hafazifai la! Asha, zinafaa kwa
kutakujua umemkataa shetani, pia unamkanyaga
shetani.
NINI MAANA YA SIFA.

Sifa maana yake ni KUTUKUZA, KUADHIMISHA,
KUINUA JUU KITU AU MTU kwa jinsi alivyotenda.
Tunapomsifu Mungu, TUNAMTUKUZA,
KUMUADHIMISHA, KUMUINUA JINSI ALIVYO KWA
MATENDO YAKE ATENDAYO. 
Tusome pamoja kitabu cha 1 Nyakati 29:10-13 maandiko yanasema hivi;"Kwa hiyo Daudi akamuhimidi
BWANA, mbele ya mkutano wrote.....Ee BWANA,
Ukuu ni wako, na uweza, na utukufu, na kushinda..."
Daudi anatoa sifa hizo kwa Mungu baada ya Israeli kutuo
Mali zao kwa utumishi wa nyumba ya Mungu.Maana
wameteoa kwa uwezo wa Mungu.
Pia Israeli wanamsifu Mungu baada ya kuvuka bahari
ya shamu walipokuwa wakitoka Misri, tusome  Kutoka 15: 1-21 maandiko yana sema; " Ndipo wana wa Israeli
wakamwimbia BWANA wimbo huu wakanena, na
kusema.."NITAMWIMBIA BWANA, KWA MAANA
AMETUKUKA SANA; FARASI NA MPANDA FARASI
AMEWATUPA BAHARINI...;
Kwa hiyo maana ya sifa ni kumgusa Mungu yeye peke yake katika uzuri wake au matendo yake,
na anaposifiwa ndipo  Mungu ufurahi na ndiyo maana
anasema,,," ANAKETI KATIKATI YA SIFA "
Kama Mungu anaketi katikati ya sifa maana yake
 wakati wa kumsifu yeye lazima uwahudumia watu wakati wa sifa.
Hivyo
usiweke mizahaa kwenye kwenye kumsifu Mungu.

NINI HUTOKEA MUNGU
ANAPOPEWE SIFA

Uwepo wa Mungu ushuka anaposifiwa.Uwepo wa Mungu 
tunaweza kusema ni (UTUKUFU WA MUNGU)
Utukufu huo unajidhihisha kutoka ulimwengu wa
Roho unakuja ulimwengu wa mwili.
Yesu alipokuwa mlimani na wanafunzi wake Petro, Yohana na Yakobo
waliuona utukufu wake kwa macho ya damu na
nyama.
Pia wana wa Lawi Asafu na Hemani na Yeduthuni na
wana wao walipokuwa wanamsifu Bwana Utukufu ukashuka. Ebu tusome pamoja kitabu cha
2 Nyakati 5:12-14 maandiko yanasema,,"...Nao wakipaza sauti pamoja na
panda na matoazi na vinanda wakimsifu Bwana
wakisema.." KWA KUWA NI MWEMA; KWA MAANA
FADHILI ZAKE NI ZA MILELE; ndipo nyumba ikajawa
na wingu, naam, nyumba ya BWANA; hata makuhani
hawakuweza kusimama kufanya Huduma yao kwa
sababu ya lile wingu; kwa kuwa nyumba ya Mungu
imejaa utukufu wa BWANA.

Wasomaji wa Biblia wanaelewa jinsi Paulo na Sila walipomsifu Bwana UWEPO
(UTUKUFU) ukashuka, misingi ikatikasika gereza
lote ni minyororo ikafunguka..oh! Haleluya.
Na wewe uwapo kanisani  kwako ukimsifu katika
roho na kweli lazima vifungo katika maisha yako
vufunguke kwa sababu Mungu anayeketi katika sifa lazima ashuke katika utukufu wake na kukuhudumia.

KAMA HUJAOKOKA OKOKA SASA BAADA YA KUFA HUKUMU.(Waebrania 9:27)
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. 
MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. 
MUNGU akubariki sana .
 Ni mimi ndugu yako 
Emmanuel Kamalamo 
Injili Kwa Kila Nyumba.

ekamalamo@gmail.com 

MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili


Hakuna maoni:

Unordered List

Download

Contact Us

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *