Inri Cristo, 66, akiongea na wanafunzi (wafuasi) wake nje ya kanisa lake liliopo Brasilia nchini Brazil.
Mwana wa mungu Inri - neno la kilatino ambalo maana yake ni 'Yesu wa Nazareti', 'Mfalme wa wayahudi' ana amini kwamba mahali kanisa lake lilipo ndo Yerusalemi Mpya'.
Hawa ni baadhi ya wanafuzi wa Inri Cristo ambao huishi hapo hapo kwenye eneo la kanisa. Wengi wa wawashiriki hao wamekuwa wakijulikana na Inri kwa zaidi ya miaka 20.
Pamoja na kwamba ni nyumba ya Yesu na makao makuu ya dehebu la Inri lakini bado hutumia mbwa kwa aajili ya kumlinda.
Wafuasi wa Inri Christo ambao ni wanawake huvaa nguo za blue ambazo zina logo ya kanisa hilo, zenye kamba kiunoni na kofia za kufumwa.
Inri Cristo huwahubiria waumini wake kila Jumamosi asubuhi kutoka mimbara yake kwenye mji wake 'Mpya wa Yerusalem'
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni