Jumanne, 14 Aprili 2015

SOMO: MTU KUPONYWA AU KUWEKWA HURU.

              
Daniel Deliverance
    
                                        SHALOM MTU WA MUNGU ALIYE HAI.
                                       NAKUSALIMU KATIKA KRISTO YESU.
                           SOMO:  MTU KUPONYWA AU KUWEKWA HURU.
Uhuru ni kutoka katika UTUMWA au kufungwa katika Agano la aina Fulani.
Mfano = Ugonjwa,Njaa,Ujinga,Uzembe Nk.
Watu wengi sana wako chini ya Kongwa la utumwa wakiwa wanajua au pasipo kujua lakini wako utumwani wakimtumikia bwana Yule katika Agano lake bila kujijua. Njia hizo zote zilitokea wakati ule pale Adamu alipopoteza mamlaka kule EDENI, sasa tumefanyika kuwa watumwa lakini kunayo kanuni ya kutoka hapo nayo ni UTAMBUZI + NEEMA.
UTAMBUZI - Ukitambua mwenyewe kuwa hiki ni kifungo ukachukua jukumu la kukikata hapo utashinda hilo kongwa la utumwa uwe wa Ugonjwa,Njaa,Ujinga,Uzembe nk. Lakini hii ni njia nzuri sana maana ufahamu wako utapata afya ya kukufanya utambue huyo bwana hakuwa halali maana yuko yeye aliyeviweka vyote chini ya miguu yake.
NEEMA –Neema huja pasipo kuleta jitihada yoyote hii inaweza kuondolewa pia maana hauna huo utambuzi unaweza ombewa ukafunguka lakini mara ukarudi tena kule kule pasipo kujua hapa yahitajika ziada baada ya neema ukasimama sawasawa kwa kuwa yuko Yule wivi azungukaye na kutaka kukuangusha tena,ndio maana Yesu unakuta anawaambiwa wale aliowaponya umesamehewa dhambi zako usitende dena dhambi lakini huu utambuzi wa kutokutenda dhambi hana. Hivyo neema ni ya MUDA kitambo tu baadae itafutwa lakini juhudi ni ya kudumu maana umeshakuelewa nawe utasimamia hapo.
Ndugu yangu katika Kristo Yesu wacha nikwambie jambo moja ambalo nimepewa ujumbe wake jumapili hii kwanini unapitia hapo ulipo,au tunapitia hapa tulipo ni kwa kuwa tumeacha kuombea wengine bali tunajiombea wenyewe tu,Mungu amesema nami utapita mahali pagumu sana kama wewe unajiona ni bora na unajiombea mwenyewe lakini huombei wengine hivyo anza kwa kufanya TOBA ya kutokuombea wengine kwanza ndipo nami nitafanya mambo yako unayohitaji.Nilimuona Mungu mara nyingi sana akiwa pamoja nami katika kazi na mambo yangu lakisa sasa ameniacha na kunipitisha katika magumu ili nijifunze kitu namshukuru Roho mtakatifu amenifunulia hili na sasa nimemuona Mungu alivyo mwema anza leo ili upate nawe yale mahitaji yako.
Najua unaye rafiki,jirani,ndugu,wanajumuia,wafanyakazi wenzako nk, wanao pitia shida na mambo mbalimbali magumu ombea hayo ya kwao nawe Mungu atafanya yako.
Nimeona nikushirikishe ujumbe huu ili upokea sasa na mapenzi ya Mungu, Mungu wa mbinguni akubariki sana.


           Usimwache BWANA YESU siku zote za maisha yako.
 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana .
                 Ni mimi ndugu yako Daniel Deliverance.
                         Mob:0754416600 
                        Email: ermbuya@yahoo.com 
           MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

                Injili Kwa Kila Nyumba.By Hezron Mwanafunzi Wa Yesu


Hakuna maoni:

Unordered List

Download

Contact Us

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *