Jumatatu, 4 Mei 2015

WANAWAKE MSIKUBALI KUPIGWA PICHA ZA UCHI

WANAWAKE MSIKUBALI KUPIGWA PICHA ZA UCHI
Kikawaida linapotokea jambo baya katika jamii basi ni wajibu kuelimishana na kukatazana mabaya na machafu yanayofanyika ili jamii iepukane na maafa na matatizo yanayokuja na hayo mambo mabaya.
Hivi siku za karibuni kumekuwa kuna kitendo cha kishenzi na cha kudhalilishana kinaendelea katika familia zetu na jamii zetu,jambo hili ni aibu,fedheha halimo kwenye utamaduni wetu,halimo kwenye utu,halimo kwenye mila,halimo kwenye desturi zetu,halimo kwenye silka zetu wala halimo kwenye thakafa za zetu.
Kumekuwa kuna mtindo wa kuwapiga wanawake picha za uchi au kuwarikodi video na kuzisambaza katika mtandao au kupitia kwenye simu kwa kutumia applications mbali mbali kama vile WhatsApp.
Hivi karibuni kuna video ambayo imesambaa kila pembe ambayo inaonesha mtoto wa kike wa miaka kumi na tano akirikodiwa uchi wa mnyama na mwanamme anayeelekea kuwa ni mtu mzima na mkubwa kuliko huyo mwanamke,katika video hiyo mwanamke ndio anaonekana uchi wa mnyama kama alivyozaliwa lakini mwanamme haonekani.Sisi binafsi tumeiyona video hio na kweli inatia unyonge na inasikitisha sana kuona kuwa Tanzania imefikia kiasi hiki cha watu kuwarikodi watoto wadogo na kusambaza video,au watu kuwarikodi wake zao na baadae video kusambaa mitaani kwa kila mtu kuiyona.
Ama kwa hii video ya huyu mtoto wa miaka kumi na tano,kama wewe uliemrikodi uko hapa unatembelea page hii ya INJILI KWA KILA NYUMBA na unasoma haya ambayo tunayaandika basi tunapenda kukwambia kwamba wewe sio mwanamme kamili,wewe ni bwege na mlaanifu,wewe hasidi na fataani na mkosefu wa adabu ulokosa radhi za wazee,wewe ndio katika wale waliopindukia mipaka,wewe ni katika majuha ambao wamepotea,wewe ni mpuuzi ambae unatia aibu kwa wanaume wote duniani,hebu jiulize nini lengo lako lilikuwa ulipokuwa unamrekodi yule mtoto?Ulimrikodi ili umkashifu au ulimrikodi ili uonekane kwamba wewe ni shababi?Basi kwa taarifa yako ulichokifanya ni kitendo cha kishenzi na udhalilishaji na mwanamme mwenye kujali na mwenye akili zake hatomrikodi mwanamke na kusambaza picha na video kwa watu wengine.na zaidi kuliko yote unapofanya ubaya duniani basi jua kwamba unajifanyia mwenyewe na juwa kuwa unapokula kuku wa mwenzio basi miguu itakuwelekea.
Kwa ufupi umemvunjia staha yule msichana na pia umemvunjia heshima na pia umemuharibia maisha yake,na pia umeikashifu familia nzima yake,na pia umemvunjia masomo yake.
KWA NDUGU ZETU WANAWAKE
Tunakuombeni ndugu zetu wa kike kwa ihsani zenu,tafadhalini msikubali kurikodiwa au kupigwa picha za uchi,ikiwa mtu mumeo au mwanamme wako au rafiki usikubali na kataa kata kata kurikodiwa au kupigwa picha za uchi,kwani kuna leo na kuna kesho na wala usijipige picha mwenyewe ukazituma kwa mtu yoyote yule hata akikulaghai kiasi gani,jua fika kuwa picha hizo za uchi zitakapotoka basi maisha yako umeyaharibu,hutopata kazi yenye staha na wala wewe mwenyewe pia hutakuwa na staha.
Mwanamme akikwambia anakupenda na umtumie picha mwambie aje kukuowa ili ataona na atapata kugusa kila kitu,na kina mama na kina baba zungumzeni na watoto wenu waelimisheni juu ya jambo hili na jengine,siku chache zilizopita tulizungumzia kuhusu umuhimu wa wazee kutumia muda wao na watoto wao kuwaelimisha,wazee lazima mupunguze kukaa maskani na kwenda kuzungumza ujinga,ukweli wa mambo ukienda maskani au kwenda kucheza karata hupati lolote la faida sana utazungumza utumbo siasa na ujinga,wakati kama ungelikaa kwako ukazungumza na watoto wako ukawasaidia kazi shule mkabadilishana mawazo wewe na mkeo basi utapata faida zaidi kuliko kwenda kuzungumza ujinga kibarazani.
Na nyinyi wanawake madada zetu na mamama zetu mjitulize,muwache choko choko na mupunguze kusengenyana,ukimuona mwenzako kanyolewa wewe tia maji,ukiona mwezako kaharibikiwa basi omba  kwa wako na wa wenzako kwa sababu haya hayana mmoja.Ukweli wa mambo sisi watu wa Tanzania wengi wetu tunapenda wenzetu waharibikiwe ili tupate kucheka pembeni na kusengenya,huo ndio ukweli tukinuna au tusinune lakini wenyewe tunajijua kila mtu mdomo mrefu,kila mtu anajuwa yeye,binaadamu mwenzako akikukera kidogo baada ya kumueleza kuwa kakukera utamuanika kwenye facebook,utamnyamba na kumtukana na kumtolea aibu zake utamvua nguo mpaka ulimwengu mzima ujuwe,wakati kama ungempigia simu au ukazungumza nae ukamwambia kuna kitu umekifanya sijakipenda basi ingekuwa bora au ungekaa kimya ukamsamehe na kumuombea  na kumsitiri aibu zake ndio ingekuwa bora zaidi,tunayaona humu kwenye facebook kuna watu wanaonewa wao tu,wanaonewa choyo wao tu,hebu jiulize ndugu yako kwa nini unaonewa choyo na kwa sababu gani?Kama unajiona mzuri basi kuna milioni wazuri kuliko wewe kama unajiona tajiri kuna matajiri mamilioni kuliko wewe kwa hio tulia sali omba Mungu na waombee wenzako.Tujiulize siku gani umemuona mwenzako au mwanawe anaeharibikiwa ukasaidia au ukamuombea  aongoke?
KWA WALE AMBAO WAMELETEWA VIDEO YA MTOTO WA MIAKA KUMI NA TANO.
Kwa ihsani yako msitiri mwenzako msitiri mtoto wa mwenzako,ifute haraka wala usimuoneshe mtu mwengine kwani hakika Mungu  atakusitiri.Sio vizuri kufichuliana aibu za mwenzio.
Sehemu yote ile yenye uonevu na uharamia na dhambi zilizoruka mpaka basi siku zote shida itaongezeka,uzinzi,riba,wizi,ulevi,ushirikina,uhasidi,ufitina,unyanyasaji uwongo mambo haya yakishamiri basi Mungu kaahidi mambo matano yatatokea na moja la mwanzo ni kupata kiongozi aliekuwa dhalimu,na haya leo tunayaona mbele ya mamcho yetu,Watanzania tunapigwa kila leo na serikali,huwezi hata kusema kile ambacho unachokitaka askari wamekupiga,jambo la pili ni umasikini na tunaona sisi kila siku hali za maisha zinazidi kuwa duni,kazi hamna watu wanazidi kuwa mafukara na wezi umeshamiri,la tatu ni mvua kutokuwa na barka na haya tunayaona aidha hakuna mvua na ikija basi mafuriko.
Watanzania wenzetu lazima tubadilike,na kubadilika kuaanza ndani ya nyumba zetu,tupendanena tuwapende watoto wetu na pia tukemee vitendo viovu na tuombeane 
injilikwakilanyumba.blogspot.com
                                                           by
                                        INJILI KWA KILA NYUMBA

Hakuna maoni:

Unordered List

Download

Contact Us

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *