Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Ally
Mwalimu akiwa katika Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa
kuhusu Hali ya Wanawake ( CSW). Kushoto kwake ni Mwakilishi wa Tanzania
wa Kudumu Katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manong.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Ally
Mwalimu ( Mb) ametoa hutuba kwa niaba ya Kundi la Nchi za Afrika wakati
wa ufunguzi wa Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu
Hali ya Wanawake ( CSW). Mkutano huu wa wiki mbili .
unawakusanya
wawakilishi kutoka serikali mbalimbali duniani na Asasi za Kiraia
ambapo hujadiliana na kubalishana uzoefu na kuelimishana kuhusu hatua
mbalimbali ambazo serikali zao zinachukua katika kuboresha maisha ya
mwanamke na mtoto wa kike.
Wakati
mamia ya wanawake kutoka serikalini na Asasi za Kiraia wakiwa
wanakutana hapa Umoja wa Mataifa kwa mkutano wao unaojadili hali yao
katika maeneo mbalimbali. Mamia mengine ya wanawake hususani wale wa
Afrika wanaendelea kukumbana na changamoto lukuki zinazowarudisha nyuma
kimaendeleo.
Ni
wanawake hao wanaoishi katika nchi zenye migogoro, vita visivyokwisha,
wenye kukabiliwa na uhaba na ukosefu mkubwa wa chakula, maji safi na
salama, matatizo yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi, ndio ambao
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto, Mhe. Ummy
Ally Mwalimu(Mb) ameitaka jumuiya ya kimataifa kuongeza kasi ya
ushirikiano ili malengo mapya ya maendeleo endelevu (Agenda 2030) yaweze
kuwafikia.
Waziri
Mwalimu ametoa wito huo jana jumatatu, wakati alipotoa hutuba kwa niaba
ya nchi za Afrika katika siku ya kwanza ya Mkutano wa 60 wa Kamisheni
ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya wanawake (CSW) ambao umeanza hapa
Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Ally
Mwalimu akitoa hotuba katika Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa
Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake ( CSW).
Changamoto
hizo pamoja na nyinginezo nyingi zikiwamo kutopata fursa ya huduma za
afya ya uzazi salama, elimu na usawa wa kijinsia zinamfanya mwanamke wa
Afrika ashindwe kushindana na wanawake wenzie hususani wale walioko
katika mataifa yaliyoendelea.
Waziri
Mwalimu ambaye anaongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huu wa wiki
mbili, alitoa hotuba hiyo kwa niaba ya nchi za Afrika kutokana na kwamba
Tanzania kupitia Uwakilishi wake wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa
Mataifa ni Mwenyekiti wa Kundi la Nchi za Afrika kwa mwezi huu wa March.
Amewaeleza
washiriki wa mkutano huo waliofurika katika Ukumbi Mkuu wa Mikutano wa
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kwamba ingawa pamekuwapo na makubaliano
na mapendekezo mengi kuanzia yale yaliyofikiwa huko Beijing, bado
mwanamke anayeishi katika nchi zenye migogoro na vita barani Afrika
ataendelea kuachwa nyuma na hivyo kukosa fursa ya kushinda na wenzie.
“
Ingawa vita, ukame wa kutisha, ukosefu wa chakula, ukosefu wa maji
safi, ukichanganya na ukosefu wa fursa za kiuchumi, kijamii na kisiasa
ni matatizo yanayowakabili watu maskini lakini mwanamke ndiye
anayeathirika zaidi,” alieleza Waziri Mwalimu.
Na
kuongeza kwamba Afrika inaendelea kutilia mkazo hoja ya kuwashirikisha
wanawake katika majadiliano na utoaji wa maamuzi katika masuala
yanayowagusa yakiwamo masuala yanayohusu mabadiliano ya tabia nchi na
usuluhishi wa migogoro.
Alieleza
kwamba, nchi zinazoendelea na zilizoendelea zinapashwa kuongeza kasi ya
ushirikiano na ubia baina yao ili kufanikisha utekelezaji wa Agenda
2030), Makubaliano juu Mabadiliko ya Tabia nchi yaliyofikiwa huko Paris
Ufaransa mwaka jana na makubaliano yaliyofikiwa na waafrika wenye
kupitia Ajenda 2063 , ili katika umoja wake dunia basi iweze kumwondoa
mwanamke na jamii nzima kutoka hapa ilipo na kufikia hali bora zaidi ya
maisha.
Kama
hiyo haitoshi Waziri alisema, Afrika inaamini pia katika uwezeshwaji wa
Sekta binafsi, kupanua wigo wa ujasiliamali kama njia mojawapo ya
kukuza uchumi endelevu , usawa wa kijamii, usawa wa jinsia, ulinzi wa
mazingira na uwezeshaji wa mwanamke.
Mada
kuu ya Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya
Wanawake, ni “Uwezeshaji wa Wanawake na uhusiano wake na Ajenda 2030.
Awali
akizungumza mwanzoni mwa mkutano huu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,
Ban Ki Moon amasema tangu alipoingia madarakani mwaka 2006 amejjitadi
kuongeza nafasi za viongozi wanawake katika Idara za Sekretarieti ya
Umoja wa Mataifa.
Akitilia
msisitizo hoja na haja ya kupanua wigo wa wanawake kushika nafasi
katika ngazi za juu za maamumizi, Ban Ki Moon amesema, ingawa nchi
nyingi zimejitahidi sana kuongeza ushiriki wa wanawake katika nafasi za
juu za uongozi bado kuna Nchi Tano ambazo hazina wanawake katika Mabunge
yao ili hali Nchi nyingine 7 hazina mawaziri wanawake katika serikali
zao.
Naye
Rais wa Baraza Kuu la 70 la Umoja wa Mataifa Bw Monges Lykketoft,
akizungumza wakati wa mkutano huo, pamoja na kusisitiza umuhimu wa
utekelezaji wa Agenda 2030 ambayo ameitaja kuwa ni jumuishi ameendelea
kupigia chapuo la kutaka Katibu Mkuu ajaye wa Umoja wa Mataifa awe
Mwanamke.
Na Mwandishi Maalum, New York
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni